Karibu

Cholemu Investiment Limited ni kampuni iliyoanzishwa mwaka 2017 jijini Dar Es Salaam na kusajiliwa chini ya sheria ya makampuni ya mwaka 2002 nchini Tanzania na baadae kupata kibali cha kufanya shughuli za upimaji na uuzaji wa ardhi kwa watu binafsi, vikundi na taasisi kwa njia ya mkopo ndani ya eneo lote la nchi ya Tanzania.

Huduma zitolewazo na kampuni

 • uuzaji wa viwanja na mashamba

 • utoaji wa mikopo ya viwanja na mashmba

 • upimaji wa viwanja

 • utengenezaji (uchoraji) wa ramani

 • upangaji wa miji na makazi

 • ushauri na muongozo juu ya ujenzi

Lengo la Kampuni

Kuuza mashamba na viwanja vilivyopimwa kwa njia ya mkopo.


Dira ya kampuni

Kuwa muuzaji bora wa viwanja na mashamba kwa njia ya mkopo katika jiji la Dar es Salaam na Tanzania kiujumla.


Wateja/Walengwa

Wateja ambao tumewalenga katika biashara hii ya uuzaji wa viwanja vilivyopimwa kwa njia ya mkopo ni watu wote wenye kipato cha kati ambao ni vigumu kujikusanyia pesa nyingi kwa wakati mmoja. Watu hao ni kama vile; wafanyakazi wa idara za serikali, wafanyakazi wa taasisi binafsi, wafanya biashara wadogowadogo na wakulima wa kipato cha kati ambao kipato chao hawawezi kukilimbikiza kufikia kununua viwanja au mashamba kwa malipo ya mkupuo.

Ufafanuzi kuhusiana na ardhi

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne katika kuchangia maendeleo. Vitu hivyo ni Ardhi, Siasa Safi, Uongozi Bora na Watu. Kwa msingi huu Mwalimu alimaanisha kwamba, ardhi ni miongoni mwa misingi madhubuti ya Maendeleo. Hivyo basi, kama wananchi watapatiwa ardhi kwa kadiri inavyotakikana na kuitumia kwa ufanisi basi ardhi itawakwamua kiurahisi katika wimbi la umasikini na kuwasaidi kuwa na rasilimali ya kutosha kwa ajili yao na vizazi vijavyo. Kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 2002; ardhi inajumuisha nafasi ya juu ya ardhi pamoja na ile iliyopo chini yake na vitu vyote vilivyomo ndani yake isipokuwa madini au mafuta yaliyopo katika ardhi hiyo. Hii inajumuisha pia vitu vya asili vinavyoota au kuoteshwa katika ardhi hiyo, majengo pamoja na ardhi iliyofunikwa na maji. Sheria hii paoja na sera na kanuni zake zinaeleza kwamba ardhi yote ya Tanzania ni mali ya umma ikiwa chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano kama mdhamini kwa niaba ya wananchi na kuhakikisha kuwa haki zilizopo au umiliki ambao umekuwepo tangu awali unatambuliwa na kulindwa.

Umiliki wa ardhi kwa mujibu wa sheria

Kwa mujibu wa sheria za ardhi, kila raia wa Tanzania ana haki ya kumiliki ardhi. Kumilikishwa ardhi si hisani bali ni haki ya kila raia ya kisheria na kikatiba. Hivyo kila mwananchi anapaswa kuonyeshwa na kuwezeshwa ni kwa jinsi gani ataweza kumiliki ardhi.

Tanzania ni nchi iliyobahatika sana miongoni mwa nchi zilizo katika eneo la afrika mashariki kwa kuwa na ardhi tele ambayo kila raia wa kizazi cha sasa na kijacho anao uwezo wa kumiliki ardhi pasipo na tatizo lolote. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kwamba katika nchi tano za afrika mashariki 51% ya eneo la ardhi linachangiwa na ardhi kutoka nchi ya Tanzania, hii inatoa picha ni kwa namna gani kuna utajiri wa ardhi katika nchi hii kwa raia wake.


136027

BRELA NUMBER

2643879

LESENI NAMBA: B

Wateja wetu

 • Naishukuru sana kampuni ya Cholemu investment ltd kwa kuniuzia kiwanja kizuri kilichopimwa na mipango miji.

  Mussa Mlemwa
 • Asanteni sana Cholemu investment ltd kwa kunikabidhi hati ya kiwanja changu .

  Naomi Joel
 • Nimezipenda sana huduma zenu, na ningefurahi kufanya biashara na nyinyi mwara nyingine tena

  Fatma Said

Mkataba wa mauziano ya viwanja na mashamba

Mkataba wetu wa mauziano umezingatia sheria, haki na wajibu wa wateja wetu. Pia umehakikiwa na mwanasheria. Tunakuomba ubonyeze hapo chini ili kuweza kuudownload na kuupitia kwa kina zaidi

Our Team

MARIAM
MHAGAMA

Operation Manager

SWAUMU
MOHAMEDY

Marketing Manager

RUTOZ
YAHYA

Project Manager

SAM
SIMON

Town Planner/Surveyor

HAROUN
BUNGA

I.T Technician

2018 | This Website Designed by PUSH DIGITAL